Der Spiegel lamkomalia Ronaldo kwa ubakaji

Muktasari:

  • Gazeti la uchunguzi la Der Spiegel la Ujerumani limekataa kuomba radhi na kusisitiza kuwa linao ushahidi wa kutosha kuithibitishia mahakama kuwa mwanasoka nyota wa Ureno anayeitumikia Juventus, Cristiano Ronaldo alimbaka Kathryn Mayorga walipokutana hotelini mjini Las Vegas mwaka 2003.

Munich, Ujerumani. Gazeti la uchunguzi la Der Spiegel, la nchini Ujerumani limeendelea kusisitiza kuwa halitaomba radhi kwa kuwa linao ushahidi wa kuutoa mahakamani kuwa mshambuliaji mahiri wa Juventus raia wa Ureno, Cristiano Ronaldo alibaka.

Gazeti hilo lililokuwa la kwanza kuibua kashfa hiyo, lilitakiwa na upande wa Ronaldo kuomba radhi na kukanusha habari hiyo, lakini limemesisitiza kuwa halitaomba radhi na liko tayari kwenda kuthibitisha madai yao mahakamani kwa kuwa lina nyaraka zaidi ya 100.

Wakili wa Ronaldo, Peter Christiansen, alilitaka gazeti hilo kuomba radhi na kukanusha habari hizo ama wasubiri kuburuzwa mahakamni kwa kosa la kumchafua mteja wake, kuhusiana na kuibua tuhuma ya kumbaka Kathryn Mayorga katika hoteli mjini Las Vegas mwaka 2009.

Christiansen alisema namna ambavyo gazeti hilo liliandika kwamba Mayorga alimkatalia Ronaldo akisema hapana. Hapana. Acha …kana kwamba walikuwepo eneo la tukio na kushuhudia kila kitu.

Wakili huyo wa Ronaldo anadai kuwa anaamini gazeti hilo limejipanga kutumia nyaraka za uwongo mahakamani ili kufanikisha malengo yao ya kumchafua mteja wao na medani nzima ya soka kwa manufaa yao binafsi.

“Tumewasikia upande wa Ronaldo lakini tunachosema ni kuwa habari hiyo ni kweli kwa mujibu wa nyaraka tulizonazo na kama wanabisha basi wasubiri tutazitoa wakati wa utetezi wetu mahakamani,” lilisema Der Spiegel.

Mayorga amekua na kauli tata kuhusu sababu za kukaa kwake kimya tangu kuibuka kwa kadhia hiyo mwanzo alidai kuwa aliahidiwa pesa ndefu na lakini baadaye akasema kuwa alishindwa kufichua kwa kuogopa aibu na fedheha mbele ya jamii. 

Kashfa hiyo ya ubakaji kwa Ronaldo inamyumbisha sana nje ya uwanja kwani tayari kampuni mbili zinazomdhamini ikiwemo Nike zimesema zinachunguza tukio hilo la likithibitika litaachana naye.

Mbali ya kampuni hizo pia klabu yake inayumbishwa na kashfa hiyo kwani baada ya kufichuliwa wiki iliyopita, hisa za Juventus ziliporomoka kwa wastani wa asilimia kumi.