England kugomea Kombe la Dunia

Muktasari:

Kocha England ashtushwa taarifa za sumu Urusi

Kocha wa timu ya taifa ya England, Gareth Southgate amesema kwamba nyota wa kikosi chake wataamua wenyewe iwapo wapo tayari kwenda kucheza fainali za Kombe la Dunia mwaka huu au la.

Kauli hiyo ameitoa kutokana na kuwapo hofu ya kupewa sumu iliyotokea kwenye mji wa  Salisbury

Kocha huyo wa England amesema kwamba hatamlazimisha mchezaji yeyote kwenda kucheza Urusi iwapo hayupo tayari juu ya usalama wa afya yake.

Southgate amesisitiza kwamba wachezaji hao wataamua wenyewe iwapo wataona inafaa kwenda au kutakwenda, lakini kwa upande wake hatamlazimisha mchezaji yeyote.

Wanasiana nchini humo wameshinikiza kufanyika kwa uchunguzi baada ya kiongozi huyo wa zamani wa Russia pamoja na binti yake kupewa sumu.

Hata hivyo, Boris Johnson alionya kwamba maandamano yoyote ya England kupinga Kombe la Dunia yatawaathiri wachezaji na mashabiki.

Waziri Theresa May alitembelea eneo la Salisbusy jana Alhamisi ili kujione hali halisi.

Hata hivyo, Southgate alisisitiza kwamba England itatuma naofisa wake wa uchunguzi kipindi hiki cha kiangazi ili kujiridhisha  hali ya usalama wa chakula.