Feisal amduwaza kocha Taifa Stars

Muktasari:

 

  • Kocha wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike ameshangazwa na kipaji cha mchezaji wa kiungo wa Yanga Feisal Salum, alichokionyesha katika mchezo wa kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika dhidi ya Cape Verde.

Dar es Salaam. Kocha wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike, amemtaja  Feisal Salum ‘Fei Toto’ ni mchezaji wa aina yake katika medani ya soka nchini. Amunike alisema hakuwahi kufikiri kama mchezaji huyo wa Yanga ana kipaji cha soka.

"Sikuwahi kumfikiri kama ana kiwango bora namna ile kwa sababu katika mazoezi anacheza utadhani anafanya masihara,” alisema Amunike.

Feisal alionyesha ubora alipoingia kujaza nafasi ya Mudathir Yayha katika mchezo ambao Stars ilishinda mabao 2-0 dhidi ya Cape Verde.