Thursday, September 14, 2017

Flaviana Matata awaponda wanaofuatilia wembamba wake

 

By Frank Ngobile

Dar es Salaam. Mwanamitindo na pia mrembo ambaye kazi zake nyingi anazifanya kwa Sauzi “hivi karibuni aliachia povu zito kwa watu ambao wamekua wakimsema kuwa anazidi kuwa mwembamba.

Katika akaunti zake katika mitandao ya kijamii, watu wamekuwa wakimsema kua mwanadada huyo anazidi kuwa mwembamba na hivyo inabidi awe anakula na si kujinyima msosi ili kuzidi kuuweka mwili wake kimwanamitindo zaidi.

Flaviana aliandika “Kiukweli watu inabidi wajifunze kudili na mambo yao na kujali mambo ya maana zaidi. Nimechoka na ushauri wa ajabu eti “NAHITAJI KULA” mnaonipa kwenye komenti, kwani nani ambaye kawaambia mi sili? Watu wengine tupo hivi hivi na tunajivunia. Nawaombeni mtunze nguvu zenu na hayo maoni yenu pia. Nina furaha kwa mwili wangu ulivyo na ndicho nachojali,” alisisitiza.

 

-->