Chanongo amaliza programu maalumu Mtibwa

Saturday November 11 2017

 

By DORIS MALIYAGA

WINGA wa Mtibwa Sugar, Haruna Chanongo amemaliza programu maalumu ya mazoezi na sasa ameungana na wenzake baada ya kukosa mechi zote tangu msimu ulipoanza.

Chanongo amepewa programu hiyo ambayo alikuwa anaanza kufanya mazoezi yake binafsi mchana saa tisa hadi 12, na baada ya kumaliza hiyo, sasa anafanya pamoja na wenzake.

Kiungo huyo aliyeichezea Simba kwa mafanikio miaka ya nyuma, alipewa programu hiyo baada ya kupona majeraha ya enka yaliyokuwa yanamsumbua tangu mwanzoni mwa msimu.

Kocha mkuu wa Mtibwa, Zubery Katwila amesema: "Chanongo amemaliza programu maalumu ambayo ilikuwa ni kwa ajili ya kumwandaa akitokea kwenye majeruhi kwa sababu alikuwa muda mrefu nje na sasa ameungana na wenzake tunaendelea naye na mazoezi ya kawaida."

Hata hivyo, Zubery ameshukuru kurejea ulingoni kwa mlinda mlango huyo na akaweka wazi hali ya mlinda mlango wake,

Shaaban Hassan 'Kado' ambaye pia aliumia mwanzoni mwa msimu, bado anaendelea na matibabu.

Advertisement