Gharama gauni la harusi ya Serena Sh 700mil

Saturday November 18 2017

 

New Orleans, Marekani. Jeuri ya fedha, hicho ndicho unachoweza kusema kwa Serena Williams aliyevaa gauni la harusi ‘shera’ lenye thamani ya pauni 2.6milioni (zaidi ya Sh700 milioni) katika harusi yake na mchumba wake Alexis Ohanian.
Serena na mumewe Ohanian walitoa picha zao za kwanza za harusi yao iliyoghalimu dola 1milioni iliyofungwa Alhamisi.
Nyota huyo wa tenisi (36), alipendeza na gauni ya thamani pauni 2.6milioni iliyotegenezwa na Sarah Burton kwa mtindo wa Alexander McQueen, gauni hilo kubwa limelembwa kwa dhahabu XIV Karats jewellery. Wakati bwana harusi Alexis (34) alikuwa amevaa koti na suruali ya kijivu kutoka kwa Armani.
Ohanian aliandika katika picha yake: "Wewe ni mwanamke bora wa wakati wote, siyo tu katika michezo, ila nazungumzia kuhusu mama na mke wangu."
Katika harusi hiyo wageni wote walipewa zawadi kikombe cha kipekee cha dhahabu kutoka kwa bi harusi Williams. Meza zote za wageni zilipewa majini ya mataji 12 grand slam aliyoshinda Williams.
Wawili hao wamekuwa pamoja tangu 2015 na ndoa yao inakuja wiki 11 tu tangu walipopata mtoto wao wa kwanza, binti Alexis Olympia Ohanian Jr aliyezaliwa Septemba Mosi. Alexis ni mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Reddit.
Watu maarufu waliohudhuria harusi hiyo ni pamoja na Beyonce, Kim Kardashian, Caroline Wozniacki na Eva Longoria. Kim aliwasili kwa ndege ya kukodi akiwa na rafiki wa dada yake, Khloe, Malika Haqq na dada yake Malika, Khadija. Mrembo Caroline Wozniaci yeye aliambatana na mchumba wake mpya, staa wa NBA, David Lee.
Dada wa Serena, Venus alipiga kivazi matata kabisa, huku mama yao Oracene Price, aliyekuwa amepiga kigauni kifupi cha zambarau pamoja na koti refu kwa nje.

Advertisement