Haji Manara asherekea siku ya kuzaliwa leo

Muktasari:

Haji Manara amekuwa maarufu kutokana na kuwa mbwembe nyingi pindi anapozungumza na wanahabari kushusu masuala mbalimbali ya klabu yake.

Dar es Salaam. Msemaji wa Simba, Haji Manara leo Alhamisi anasherehekea siku yake ya kuzaliwa huku akiwashukuru wale wote waliotuma salamu za pongezi kumtakia heri ya maisha marefu.

Manara aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram akisema, “Shukrani sana kwa Allah kuniongezea umri na kunijalia afya njema, asanteni kwa ushirikiano wenu kwangu…”

Pia aliwashukuru wana Simba kwa ushirikiano wanaompa kwenye kutekeleza majukumu yake ya kila siku,  huku pia akiwakumbuka wanahabari kwa mchango wao.

Kikosi cha Simba, leo Alhamisi kitashuka Uwanja wa Taifa kupambana na Singida United kwenye mchezo wa Ligi Kuu utakaopigwa saa 10 jioni.