Hali ya Dimpoz yaimarika

Muktasari:

  • Dimpoz's alisema alianza kufanyiwa vipimo vya afya yake nchini Kenya kwa kumkata kinyama cha shingo ili kubaini kama kweli ana kansa kama ilivyokuwa imedaiwa jijini Dar es Salaam, ambako alipima aliambiwa ana ugonjwa huo.

Dar es Salaam. SUPASTAA wa Bongo fleva, Ommy Dimpoz's hali yake inaendelea kuimalika tofauti na mwanzo alipokuwa katika matatibu nchini Afrika Kusini.
Dimpoz's alisema alianza kufanyiwa vipimo vya afya yake nchini Kenya kwa kumkata kinyama cha shingo ili kubaini kama kweli ana kansa kama ilivyokuwa imedaiwa jijini Dar es Salaam, ambako alipima aliambiwa ana ugonjwa huo.
"Nilipima hospital kubwa jijini Dar es Salaam, waliniambia nina kansa, lakini baada ya kupima Kenya ndipo nikaambiwa nililishwa sumu, nashukuru Mungu kwa maombi ya ndugu zangu, Watanzania na wasio Watanzania maombi yao yamenifanya nuru yangu irudi.
"Kikuweli kwa sasa naendelea vizuri nawaomba Watanzania waendelee kunikumbuka katika maombi yao nami nirejee katika majukumu nikiwa imara kiafya,” alisema Dimpoz.