Hans Poppe aenda na gongo Djibouti

Muktasari:

  • Asema yupo katika hatua za mwishoni za uponaji na anaendelea vizuri na asisitiza mwezi huu utakuwa wa mwisho kutumia hili gongo

KAMA kuna viongozi wapenda mpira nchini, basi mwenyekiti wa Kamati ya usajili wa Simba, Zakaria Hans Poppe ni namba moja.

Unajua ni kwa nini, Hans Poppe aliamua kusafiri kwa msaada wa fimbo ya kutembea yaani gongo kutokana na maumivu ya mguu wa kulia yanamsumbua.

Pamoja na maumivu hayo yanayosababishwa na upasuaji wa maungio ya goti, aliona vigumu kuusikilizia mpira kwenye vyombo vya habari na kuamua kupanda ndege hivyo hivyo huku akichechemea.

“Nilifanyia upasuaji mwishoni mwa mwezi wa 11, kulikuwa na shida kwenye maungio ya goti yalikutana, ndiyo maana unaniona katika hali hii,” alisema Hans Poppe.