Harry Kane atajwa kuhimili muziki timu vigogo

Muktasari:

Atajwa kufikia kiwango cha kuweza kucheza klabu yoyote barani Ulaya. 

England. Mshambuliaji wa Tottenham, Harry Kane ametajwa kuwa ni miongoni mwa wachezaji waliofikia kiwango cha kucheza klabu yoyote kubwa barani Ulaya.

Mchezaji huyo amekuwa tishia England jambo ambalo limezifanya klabu mbalimbali kumtolea macho kutaka kumsajili.

Kwa sasa amekuwa gumzo barani Ulaya jambo ambalo linafanya pia thamani yake kuongezeka msimu huu.

Mchambuzi wa masuala ya soka Sun Sports Ulaya, Lothar Martthaus alisema kwamba mchezaji huyo kwa sasa anauzika Ulaya yote.