Haya ndiyo mambo yaliyomfanya Samatta afanikiwe

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta

Muktasari:

  • Kiwango cha Mbwana Samatta kimeendelea kuimalika kila kukicha huko KRG Genk hasa msimu huu wakati timu yake ikiwa inashiriki ligi ya Europer.
  • Kutokana na kiwango chake mashabiki wa timu hiyo wamemtuyngia wimbo maalumu na hii inaonyesha namna gani alivyowagusa.

Kiwango cha mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta kimendelea kuwa chachu ya klabu yake ya KRC Genk kufanya vizuri Ulaya.

Mshambuliaji huyo mwenye miaka 25 ambaye amekuwa akizivutia klabu kad-haa barani humo, amezungumza na Spoti Mikiki kubainisha yaliyojificha nyuma ya kiwango chake cha ufungaji msimu huu wa 2018/19.

Samatta akiwa Ubelgiji kabla ya kuun-gana na wenzake nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kuwania tiketi ya Afcon dhidi Lesotho, Novemba 18, anasema amekuwa akiya-fanyia mazoezi aina ya mabao ambayo amekuwa akifunga.

“Kufunga ni kazi ngumu, nimekuwa nikifanya mazoezi kwa juhudi ili kufunga aina mbalimbali ya mabao, kuna mabao mingine unakuta nafasi inatengenezwa kazi inaweza kuwa nyepesi kwa kuangalia wapi mpira naupeleka.“

Lakini kuna mengine huhitaji utulivu na mazoezi kwa maana kama hukuwahi kuyafanyia mazoezi, unaweza ukamalizia kwa kubahatisha ndio maana kuna muda huwa naingia na mpira kwenye eneo la wapinzani nikiwa na uhakika wa kufunga.

“Mara chache nimekuwa nikipoteza nafasi za namna hiyo ila nina uwezo wa kuingia na mpira hata kama kukiwa na mabeki watatu na nikaleta madhara,” anasema Samatta.

Nahodha huyo wa Taifa Stars, anasema kufunga kwa kichwa alikuwa akifanya hivyo tangu akiwa nyumbani kwa hiyo sio aina ya mabao mapya kwake na hata alivyokuwa akiichezea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DR Congo).

Atungiwa wimboMashabiki wa KRC Genk wamepa-gawa na Samatta hadi kumtungia wim-bo. Anasema ni faraja kwake kuona mashabiki wanakubali uwezo wake na kumpa heshima kwa kuwa wanamwimbia wimbo.

“Huwa nasikiliza ule wimbo wa MO Salah na mimi nimetungiwa wimbo, najiona mchezaji wa pekee,” anasema.

Samatta anasema anajivunia kuwa mchezaji wa timu hiyo kwa namna ambavyo mashabiki wanampa sapoti na anasema hata kipindi ambacho alipata majeraha walikuwa wakimtumia ujumbe wa kumtaka apone haraka.

Nyota huyo wa zamani wa Simba, anasema amekuwa akiwaheshimu mashabiki kwa kujituma kwenye kila mchezo ili kuhakikisha wanarejea mak-wao na furaha.“Namna nzuri ya kumfurahisha shabiki siku zote kwa wachezaji ni kuhakikisha timu inapata matokeo ya ushindi kwa hiyo ninatakiwa kuendelea kufunga kwa kusaidia na wezangu,” anasema Samatta.

Akizungumzia malengo yake ya kuwa mfungaji bora wa Ligi ya Ubelgiji, Samatta anaamini kwa ush-irikiano alionao na wenzake anawe-za kuchukua kiatu cha dhahabu licha ya upinzani mkali uliopo kutoka kwa washambuliaji wa timu nyingine.“Ni wazi kuwa msimu uliopita haukuwa mzuri kwangu.

Napenda kuwa mshindi, hiyo ni tabia ambayo nilikuwa nayo tangu nikiwa Mazembe, tusubiri tuone mwisho wa msimu kama nitafikia malengo hayo,” anasema.Samatta ambaye alikuwa mfunga-ji bora wa Ligi ya Mabingwa Afrika, 2015 alikuwa miongoni mwa wache-zaji muhimu TP Mazembe ambao wali-changia timu hiyo kuchukua ubingwa wa Afrika huku akiwa na mabao saba.

Januari ya 2016, alikuwa mchezaji wa kwanza kutoka ukanda wa Afrika Mashariki kuwa mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani katika tuzo za Glo-CAF ambazo zilitolewa Abuja nchini Nigeria kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano.

Samatta ali-chukua tuzo hiyp kwa jumla ya pointi 127 huku akiwabwaga wapinzani wake kipa, Robert Muteba Kidiaba ambaye alikuwa akicheza naye Mazembe kwa kuwa na pointi 88.Baada ya kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora kwa wachezaji wa ndani Afrika, Samatta alinaswa na KRC Genk kwa kusaini mkataba wa miaka minne na nusu.

Nyota huyo wa kimataifa wa Tanzania, alifunga mabao yake matatu yani hat trick kwenye mchezo wa Europa Ligi ambao ulikuwa Agosti 23 mwaka huu dhidi ya Brøndby ambao ulimalizika kwa ushindi wa mabao 5-2.