Hayo mazoezi ya Yanga Moro, Simba ijipange!

Muktasari:

  • Mpaka sasa Yanga inaonekana haina mchezaji majeruhi ukiondoa Juma Abdul na Juma Mahadhi ambao bado hawajajiunga na timu hiyo.

Morogoro. Yanga imeendelea na mazoezi katika siku ya pili leo hapa Morogoro lakini kocha wa timu hiyo ameanza na kurudisha pumzi.
Asubuhi leo Jumatano, Yanga wanafanya mazoezi katika Uwanja wa Jamhuri, ambapo kocha    Mwinyi Zahera ameonekana akianza na mazoezi ya kuongeza pumzi.
Katika mazoezi hayo Zahera ameonekana akiwawanya wachezaji wake katika makundi mawili moja likisimamiwa na mwenyewe huku lingine likisimamiwa na msaidizi wake, Noel Mwandila.
   Kocha Zahera ameonekana kutaka kuona mchezaji anakimbia kwa kufuata muda aliotaka yakiwa ni mazoezi ya mbio za kasi.
Kila mchezaji alihidhuria mazoezi hayo isipokuwa makipa pekee ambao walikuwa na mazoezi yao na kocha wao Juma Pondamali.
Mpaka sasa Yanga inaonekana haina mchezaji majeruhi ukiondoa Juma Abdul na Juma Mahadhi ambao bado hawajajiunga na timu hiyo.