Henrikh Mkhitaryan akaribia kutua Arsenal

Muktasari:

Arsenal wapo kwenye mazungumzo ya kumuongezea dau la mshahara hadi kufikia Pauni 140,000 kwa wiki.

England. Mchezaji wa Manchester United, Henrikh Mkhitaryan imeelezwa anakaribia kutua Arsenal ikiwa ni siku chache tangu klabu hiyo imnyakue Alexis Sanchez kutoka dimba la Emirates.

Nyota hiyo wa Manchester United amesema hana muda mrefu kuendelea kuwapo kikosi hapo.

Mkhitaryan ameweka wazi kwamba kwa sasa hana muda mrefu kuendelea kuwapo kikosini hapo.

Manchester United imefunga ukurasa wa usajili wa Sanchez baada ya kuipiga kumbo Manchester City. Sanchez amejifunga kuitumikia Manchester United hadi mwaka 2020

Mkhitaryan ameweka bayana kwamba kinachomuondoa United ni kutokana na mshahara kiduchu ambao haridhiki nao.