Iwobi aota kuifunga Argentina

Muktasari:

Nigeria imekuwa na ushindani mkubwa kila inapocheza mechi dhidi ya Argentina

London, England. Mshambuliaji wa Nigeria, Alex Iwobi anaamini Super Eagles itawafunga Argentina kwa mara ya pili wakati timu hizo zitakapokutana miezi michache ijayo katika Kombe la Dunia Russia.

Iwobi aliisaida Nigeria kushinda 4-2 katika mchezo wa kirafiki dhidia Argentina uliofanyika kwenye Uwanja wa Krasnodar mwezi Novemba 2017.
Timu hizo zitakutana tena wakati wa Kombe la Dunia wakiwa Kundi D na mechi hiyo itachezwa Saint Petersburg Juni 26.
“Argentina ilimkosa nyota wake Lionel Messi, lakini na sisi hatukuwa na baadhi ya wachezaji weti. Tunaamini tutaendelea kujiamini katika mchezo ujao katika Kombe la Dunia,” alisema Iwobi. 
“Hatukufungwa katika mechi za kusaka kufuzu kwa Kombe la Dunia na tunajiamini tukiwa ni vijana wenye vipaji ambao tunataka kuthibisha ubora wetu uwanjani.”
Nigeria pia imepangwa kundi mmoja pamoja na Croatia na Iceland katika mashindano hayo makubwa.