Joshua asherehekea kuzaliwa kwake kiaina

Muktasari:

  • Bondia anayeshikilia mikanda mitatu ya ubingwa wa Dunia uzani wa juu, inayotambuliwa na WBO, WBA na IBF Anthony Joshua wa Uingereza jana alisherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa staili ya aina yake kwa kuwasha mshumaa aliouita wa matumaini ndipo ukataji wa keki na hafla fupi vikafuata.  

London, England. Bondia anayeshikilia ubingwa wa Dunia uzani wa juu, Anthony Joshua, jana aliungana na marafiki na jamaa zake wa karibu kula keki ya siku ya kuzaliwa kwake.

Bondia huyo alikua akisherehekea kutimiza miaka 29, ambapo aliuwasha mshumaa aliouandaa kwa ajili hiyo huku akitamba kuwa ni wa matumaini dalili njema kwake kwamba ataendelea kumeremeta kwa kipindi kirefu kijacho.

Joshua alitwaa ubingwa huo wa Dunia baada ya kumchapa Alexander Povetkin wa Russia kwa KO na kutwaa mataji ya WBO, WBA na IBF sasa anasubiri kucheza pambano la kuunganisha mikanda atakapocheza na Deontay Wilder anayeshikilia ubingwa wa WBC.

Joshua ameshinda mapambano yake yote 22 ya ngumi za kulipwa aliyocheza huku akishinda 21 kwa KO na moja pekee ndilo ameshinda kwa pointi.

Amepangiwa kucheza pambano lake lijalo kwenye uwanja wa Wembley, jijini London Aprili mwakani, ingawa mpinzani bado hajaamuliwa lakini ni kati mmarekani Wilder aua mwingereza mwenzake Tyson Fury.