Kagere nje, Bocco, Okwi kukiwasha Kirumba

Muktasari:

Bocco, Okwi kwa pamoja msimu uliopita walifunga mabao 34 na kuipa Simba ubingwa wa kwanza baada ya miaka 5

Mwanza. Kinara wa ufungaji wa Simba, Meddie Kagere leo ataanzia benchi wakati mabingwa hao watetezi watakapoikabiri Mbao Fc kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Kagere tangu ametua Simba akitokea Gor Mahia ya Kenya ameanza katika michezo mitatu ya Ligi Kuu huku akifunga mechi mbili mabao yake matatu.

Hata hivyo katika mchezo uliopita dhidi ya Ndanda, kocha Patrick Aussems aliwaanzisha Kagere, Emmanuel Okwi na John Bocco, lakini watatu hao walishindwa kuelewana na kushudia Simba ikilazimishwa suluhu kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona kwa mara ya kwanza.

Baada ya mbinu yake hiyo shindwa kuzaa matunda kocha Mbelgiji leo ameamua kuwaanzi vinara wa ufungaji wa msimu uliopita Okwi na Bocco katika safu yake ya ushambuliaji akitumia mfumo wa 4-4-2 katika kuhakikisha wanapata ushindi.

Washambuliaji hao wawili Okwi na Bocco waliokuwa tishio kwa kuzifumania nyavu msimu uliopita bado bado hawajafunga bao lolote katika Ligi Kuu msimu huu.

 Hivyo uamuzi wa kuanzisha ni kuona jinsi wanavyoweza kurudi katika mstari wao wa ufungaji.

Picha kocha Aussems leo amemuanzisha kiungo Mzambia Clatous Chama kwa mara ya kwanza atasaidia na Mohammed Ibrahim katika kutegeneza mashambulizi huku Jonas Mkude akiwa chini yao kulinda safu ya ulinzi.

 Vikosi

Kikosi Simba: Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein, Erasto Nyoni, Pascal Wawa, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Clatous Chama, John Bocco, Emmanuel Okwi na Mohammed Ibrahim

Kikosi cha akiba: Deogratius Munish, Paul Bukaba, James Kotei, Said Ndemla, Meddie Kagere, Marcel Bonaventure.

Kikosi Mbao: Hashim Mussa, Vicent Philipo, Amos Charles, David Mwassa, Peter Mwangosi, Ally Mussa, Said Khamis, Hussein Seleman, Rajesh Kotecha, Pastory Athanas na Aboubakary Mfaume.

Benchi: Bruno Thomas, Hamimu Abdul, Yusuph Amos, Evarijestus Mujwahuki, Zamfuko Elias, Roland Msonjo na Emmanuel Mtumbuka

Waamuzi: Waamuzi: Mbao vs Simba

Katikati: Jonesia Rukyaa (Kagera), R1: Makame Mdogo (Shinyanga), R2: Martin Mwalyaje (Shinyanga)