Kajala ashangaa wanaotafuta kiki Bongo kupitia waume za watu

Muktasari:

  • Akizungumza na mwandishi, Kajala, alisema kuna watu wengi wako radhi kutengeneza kiki kama hizo za kuchukuliana mabwana lakini kwake hazitaki na zinamkera sana kwa sababu mambo hayo yameshapita na wakati na kwanza pia hayamjengei chochote kwenye jamii zaidi ya kumuharibia.

STAA kiwango kunako filamu Bongo, Kajala Masanja kwa mara ya kwanza ameweka wazi kuwa hakuna kitu ambacho anakichukia katika maisha yake kama mtu kumbambikia kiki ambazo zinahusiana na kutembea na mume wa mtu au bwana wa mtu kwa sababu haimjengei chochote kwenye jamii zaidi ya kumuharibia.
Akizungumza na mwandishi, Kajala, alisema kuna watu wengi wako radhi kutengeneza kiki kama hizo za kuchukuliana mabwana lakini kwake hazitaki na zinamkera sana kwa sababu mambo hayo yameshapita na wakati na kwanza pia hayamjengei chochote kwenye jamii zaidi ya kumuharibia.
“Kiki kama hizo sizitaki kabisa kuzisikia kwanza zinaniharibia wala hazinijengi chochote kwenye jamii yangu zaidi ya kuniletea picha tofauti kwenye jamii yangu,” Kajala alionya.

Kajala ametoa ushauri huo ikiwa kuna fukuto la Hamissa Mobetto kutangaza kwamba amezaa na Diamond ambaye ni baba wa watoto wawili kwa Zari Hassani.