Kaseba adundwa apelekwa hospitali

Muktasari:

  • Hata hivyo, pambano jingine lililokutanisha mabondia Mfaume Mfaume na Deo Samwel liliingia dosari baada ya kutokea vurugu.

Dar es Salaam. Bondia nguli Japhet Kaseba amekubali kipigo dhidi ya hasimu wake, Mada Maugo baada ya kunyukwa kwa Knock Out (KO).

Hata hivyo, pambano jingine lililokutanisha mabondia Mfaume Mfaume na Deo Samwel liliingia dosari baada ya kutokea vurugu.

Mapambano hayo yalipigwa juzi Uwanja wa Kinesi, Dar es Salaam ambapo Kaseba alisalimu amri raundi ya sita.

“Hivi tunavyozungumza niko Mwananyamala Hospitali kwa matibabu,” alisema Kaseba.

Pambano la Mfaume na Samweli lilimalizika kwa vurugu na mwamuzi Athony Rutta, alisema hakuna mshindi baina ya wababe hao na uchunguzi wa vurugu hizo umeanza.

(Imani Makongoro)