Kaseba arudi ulingoni kuzichapa

Muktasari:

  • Kaseba anayefahamika zaidi kama Champion, atapanda ulingoni kuzichapa na Karage Suba kwenye Uwanja wa Garden Mtamba Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

KAMA ulidhani bondia Japhet Kaseba ndio basi tena, pole yako. Jamaa yupo freshi na wala kiwango chake hakijashuka kama wengi wanavyofikiria na Jumapili hii atathibitisha atakapopanda tena ulingoni.

Kaseba anayefahamika zaidi kama Champion, atapanda ulingoni kuzichapa na Karage Suba kwenye Uwanja wa Garden Mtamba Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Bingwa huyo wa dunia wa Kick Boxing, atazichapa na Suba katika pambano la raundi 10 la uzani wa super middle kg 76 linaloratibiwa na mkongwe Said Yazidu.