Kaseja, Ndikumana hao KMC

Muktasari:

  • Wachezaji hao wamejiunga na KMC iliyopanda ligi kuu kwa mara ya kwanza msimu huu na wataungana na kocha, Mrundi Etiene Ndayiragije.

Mlinda mlango mwenye heshima kubwa kwenye soka la Tanzania, Juma Kaseja na Mrundi Yusuph Ndikumana wamejiunga na klabu ya KMC ya Dar es Salaam.
Kaseja aliidaki Kagera Sugar msimu uliopita na Ndikuma aliichezea kwa mafanikio klabu ya Mbao FC ya Mwanza.
Wachezaji hao wamejiunga na KMC iliyopanda ligi kuu kwa mara ya kwanza msimu huu na wataungana na kocha, Mrundi Etiene Ndayiragije.
Ndayiragije ametambulishwa na KMC baada ya msimu wa ligi kuu kumalizika na sasa atafanya kazi na timu hiyo inayomilikiwa na Manispaa ya Kinondoni.
Kaseja anakumbukwa na uwezo wake alipoingarisha Simba kwa zaidi ya miaka 10 pamoja na Taifa Stars.