Kilimanjaro Stars yarudi vichwa chini

Muktasari:

Tanzania Bara imekuwa na rekodi mbaya inapocheza mashindano hayo nje ya Tanzania

Dar es Salaam. Timu ya Taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ imerudi asubuhi ya leo kutoka Kenya ilipokuwa inashiriki mashindano ya Chalenji.

Kikosi hicho cha Ammy Ninje ambaye amekuwa akizungumzwa na wengi kuhusu uzoefu wake  kimerejea vichwa chini huku wakiambulia pointi 1 kwenye michezo minne ya Kundi A.

Kili Stars ilianza mchezo wake wa kwanza wa mashindano hayo kwa kutoa suluhu na Libya kisha ikafungwa na Zanzibar kwa mabao 2-1, pia ikapoteza  mbele ya Rwanda kwa mabao 3-1 na ikafungwa mchezo wake wa mwisho na wenyeji Kenya kwa bao 1-0.

Wakati Kili ya Ninje ikirejea,Zanzibar Herous yenyewe imepeta katika mashindano hayo kwa kutinga hatua ya nusu fainali itacheza dhidi ya Uganda .