Kocha Emery aanza mbwembwe Arsenal

London, England. Unai Emery ndiye mrithi wa Arsene Wenger katika kikosi cha Arsenal na muda mfupi tu ameahidi kuisuka timu hiyo.

Emery ameandika katika mtandao akithibitisha kupata kibarua katika klabu hiyo ya Emirates.

Emery aliyetambulishwa jana makao makuu, amempiku Mikel Arteta aliyekuwa akipewa nafasi ya kumrithi Wenger

Mchezaji huyo wa zamani wa timu hiyo anadaiwa kutoswa baada ya kuhoji bajeti ya usajili endapo atakubali kutua Emirates.

Awali, Arsenal ilizungumza na Arteta ambaye ni kocha msaidizi wa Manchester City kabla ya kuibuka Emery.

Kocha huyo wa zamani wa Paris Saint Germain (PSG), alisema amekwenda Arsenal na matarajio yake ni kupata mafanikio.

Awali, Emery aliandika ujumbe kwenye mtandao akisema ana furaha kuwa sehemu ya familia ya Arsenal.

Kocha huyo mwenye miaka 46, amepewa nafasi baada ya kukubali mfumo wa klabu hiyo wa kubana matumizi katika usajili.

Wenger aliyedumu Arsenal miaka 22 akitokea Monaco, alipendwa na vigogo wa klabu hiyo kutokana na mfumo wa kubana matumizi. bury.