Kocha Simba apata ulaji Sudan

Muktasari:

  • Msebria huyo anakumbukwa Simba kwa maneno yake makali dhidi ya  wachezaji wavivu

 Unamkumbuka Zdravko Logarusic? Yule kocha wa Simba mwenye makeke kwenye benchi la ufundi.

Jamaa limepata ulaji timu ya taifa ya Sudan baada ya kuteuliwa kocha mkuu wa timu hiyo inayojiandaa kushiriki mashindano ya mataifa bora kwa wachezaji wa ndani (CHAN) mwakani.

Sudan wamo kundi moja na wenyeji Morocco, Mauritania na Guinea.

Loga amekuwa bila klabu tangu kutemwa na Asante Kotoko ya Ligi Kuu ya Ghana mwezi Aprili na hivi majuzi alizungumza na Mwanaspoti akiomba kazi.

“Sasa hivi kuna kijibaridi kikali Ulaya ningependa sana kuwahi kazi nyingine bara Afrika nirejee kwani kule sasa hivi mazingira mazuri,” alisema.

Mbali ya Gor na Simba, pia amezifundisha klabu za AFC Leopards (Kenya), Interclube (Angola), AshantiGold na King Feisal za Ghana.