Kotei akili yote kwa Wamisri

Muktasari:

Simba imerejea katika mashindano ya kimataifa baada ya kukaa nje kwa zaidi ya miaka minne

DJIBOUTI. Kiungo wa Simba, Mghana James Kotei amesema wana kila sababu ya kuwatoa El Masry ya Misri katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika, lakini kitu kikubwa ni kujifunga kwa malengo na umakini.

Simba imeitoa Gendarmarie ya Djibouti katika mashindano hayo kwa jumla ya mabao 5-0 na hivyo watakutana nao El Masry hatua ya pili.

Alisema:"Tunashukuru tumevuka hatua ya kwanza na sasa tunakwenda ya pili. Tunakwenda kucheza mechi na El Masry si ya kubeza ni timu kubwa yenye uzoefu katika mashindano haya."

"Lakini, Simba pia si timu ndogo, ninachoamini tuna kila sababu ya kuwafunga na tukasonga mbele, lakini ili ufanikiwe jambo moja ni kuwa na malengo, kujitoa na kuongeza umakini," alisema Kotei.

"Unaposema kujitoa yaani,  kila mmoja aweke nguvu hapo akiamini hakuna litakaloshindikana, umakini ndiyo kitu muhimu kabisa."

Kotei alisema kama watafanya hivyo, hakuna kitakachowaharibia na watawashangaza watu.