VIDEO-Kotei umwambi kitu kwa Diamond

Muktasari:

Kiungo huyo Mghana yupo na kikosi cha Simba nchini Djibout tayari kwa mechi yao ya kesho dhidi ya Gendarmarie

 Kiungo wa Simba, Mghana James Kotei ni mtaalam wa kuimba Bongo Flava na nyimbo anazojua ni za Diamond.

Kotei alionyesha uwezo wake huo walipokuwa kwenye Uwanja wa Ndege ya Kenyatta, Nairobi Kenya wakati wa kubadilisha ndege kwenda Djibouti kuivaa Gendarmarie.

Mghana huyo alikuwa na wachezaji wenzake Emmanuel Okwi, Mohamed Hussein 'Tshabalala', Nicholas Gyan na Asante Kwasi.

Walimwambia aimbe ndo akaanza mambo yake na kuimba wimbo wa Diamond wa Eneka na kuwafanya wenzake wakishangilia kwa furaha.

Diamond amekuwa kivutio kwa wanamichezo wengi kutokana na aina yake ya uimbaji pamoja na uwezo wake wa kuimba.

Alipoukizwa kama anavutiwa na mwanamuziki huyo, Kotei alisema ni kweli  :"Nampenda Diamond."