Kuiona Simba, Nkana buku tatu tu

Muktasari:

  • Viingilio katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika Kati ya Simba na Nkana vyatangazwa huku watu wa hali ya chini wakikumbukwa.

Dar es Salaam. Simba imetangaza viingilio vya mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Nkana Red Devil's huku kiingilio cha chini kikiwa Sh3000.

Simba itaikabili Nkana ya Zambia katika mchezo wa marudiano wa Mabingwa Afrika utakaofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Wekundu wa Msimbazi wanatakiwa kushinda kuanzia mabao 2-0 ili kufuzu hatua ya makundi ya mashindano hayo.

Afisa Habari wa Simba, Haji Manara alisema VIP A kiingilio kitakuwa sh 20000, VIP B. Sh 10000 na mzunguko 3000.

"Tumetangaza viingilio vya chini na rafiki kwa kila mtu watu waje kwa wingi kuisapoti timu.