Kutekwa Mo kwazidi kutikisa nchi

Muktasari:

  • Dewji 'Mo' ambaye ni mmiliki wa klabu ya Simba alitekwa jana asubuhi na watu wawili ambao hadi sasa hawajafahamika wakati akienda kufanya mazoezi ya viungo, kwenye gym iliyopo katika hoteli ya Colosseum iliyopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Mwanza. Wakati hali ya sintofahamu ikiendelea kutanda baada ya kutekwa mfanyabiashara maarufu nchini na mwanamichezo, Mohamed Dewji 'Mo' na watu wasiojulikana, mashabiki wa soka jijini Mwanza wamefunguka huku wakimuombea apatikane akiwa salama.

Dewji 'Mo' ambaye ni mmiliki wa klabu ya Simba alitekwa jana asubuhi na watu wawili ambao hadi sasa hawajafahamika wakati akienda kufanya mazoezi ya viungo, kwenye gym iliyopo katika hoteli ya Colosseum iliyopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Wakizungumza na Mwananchi kwa nyakati tofauti mashabiki wa soka jijini hapa wengi wao wakiwa na majonzi, walisema tukio hilo ni la kuogopesha lakini kwa kuwa mamlaka zinaendelea kufanya uchunguzi wa tukio zima na kujua aliko wao wanaendelea kumwombea apatikane akiwa hai.

Baadhi ya wanachama hao, Salya Ludanha, Hassan Kaheshi na Juma Mlilo walisema wameumizwa sana na tukio hilo pamoja na vyombo vya dola kuendelea kufanya kazi yake, wao wanaelekeza nguvu zao katika maombi ili mfanyabiashara na mwanamichezo huyo apatikane akiwa hai.

Ludanha ambaye ni Mwenyekiti wa muda wa Klabu ya Simba Mkoa wa Mwanza, amewaomba mashabiki wa klabu hiyo, wanamichezo na watanzania kwa ujumla wao kumuombea Mo apatikane akiwa hai.

"Bado ni mapema sana lakini niwaombe mashabiki wa Simba, wanamichezo kwa ujumla wetu na watanzania kwa ujumla tumuombee Mwenyezi Mungu amnusuru na mabaya, apatikane akiwa hai, yule ni kiongozi wetu kwa hiyo watulie wakati mamlaka zikiendelea kufanya kazi yake," alisema Ludanha.

"Siwezi kuzungumza zaidi kwa sababu ni mapema ni jambo la kusubiri tu, lakini kikubwa ni kuomba dua ili aweze kupatikana akiwa salama" amesema Kaheshi.

Mazungumzo miongoni mwa wadau wa soka jijini hapa yametawaliwa na mijdala kuhusiana na kutekwa kwa mfanyabiashara huyo maarufu nchini ambaye ni mdau mkubwa wa michezo.

Jarida la Forbes ambalo limekuwa likifanya utafiti wake na kumtangaza mara kwa mara Dewji kama mfanyabiashara kijana aliyefanikiwa zaidi limeandika habari zake.

Forbes lilisema kuwa Dewji anashika nafasi ya 17 kwa utajiri unaofikia Dola1.5bilion.

Vyombo vya habari vya Uingereza, ikiwemo Shirika la Utangazaji, (BBC), Shirika la Habari la Uingereza (Reuters) na baadhi ya magazeti ya; The times, Daily Telegraph, Daily Mail, Irish Times, The Guardian na The Independent yameandika habari za Dewji.

Pia habari za Dewji zimetua Canada ikiwemo gazeti la Ottawacitizen , Voice of America, Sauti ya Ujerumani na Voice of America (VOA).

Kituo cha habari maarufu cha Marekani, CNN kimerusha habari za Dewji pamoja na kituo cha televisheni cha Al Jazeera cha Qatar kimeandika habari za mfanyabiashara hiyo.

Baadhi ya vyombo vya habari Afrika vilivyorusha habari za Dewji ni pamoja na Daily Nation na The Standard (Kenya), The Monitor (Uganda),  mitandao ya masuala ya biashara kama CBNCAfrica.com, Africaexponent.com, businessinsider.com, Zimbabwesituation.com na businesslive.com.

Dewji inaelezwa ni kati ya wawekezaji wazawa wenye sifa za kutengeneza ajira zaidi ya 20,000 Tanzania na amekuwa akiendesha biashara zake Afrika Mashariki na Kati.

Kupitia Kampuni yake ya METL Group, ameweza kumiliki viwanda zaidi ya 35 katika masuala mbalimbali ikiwemo; kilimo, uzalishaji mali, masuala ya nishati ya gesi na petroli, huduma za fedha, simu za mkononi, mashamba na maeneo ya makazi, usafirishaji, logistics and