Amri Said: Ligi ilipofikia ni pasua kichwa

Sunday February 18 2018

 

By OLIPA ASSA

KOCHA wa Lipuli ya Iringa, Amri Said amesema ligi ilipofikia ni pasua kichwa na ndio kitu kinachowafanya washindwe kutamba kwenye viwanja vyao vya nyumbani.

Amezungumzia kutoka sare na Azam FC, wao wakiwa wenyeji anasema ni ishara tosha kwamba walipofikia wanahitaji kuumiza akili ili kuwa na mwisho mwama.

"Ligi ni ngumu hakuna cha kusema umecheza nyumbani ama ugenini,tunatakiwa kupambana mpaka mwisho ili tuone kama tutafikia malengo yetu kwanza, kubakisha timu ligi kuu na kumaliza nafasi nzuri,"anasema

Kocha huyo anasema wanaendelea kuwajenga wachezaji wao kuelewa mzunguko wa pili wanatakiwa kuwa wazalengo kwa timu hivyo akili zao ziwe na utulivu wanapokuwa kwenye majukumu.

 

"Wachezaji ndio silaha kubwa ya sisi kufika kwenye pointi tunayotaka, kila wakati tunazungumza nao kuwakumbusha kujua majukumu yao kuelekea mwishoni si rahisi,wanapaswa kujitoa,"anasema.

mwisho.

Advertisement