Lwakatare Cup yapigwa Stop

Muktasari:

  • Msimamizi mkuu wa Lwakatare Cup 2017, kituo cha Mngeta, Supertus Duma alisema ligi daraja la tatu imesimamisha kuanza kwa michezo ya 16 bora ya Rwakatare Cup 2017 iliyokuwa imepangwa kwenye vituo saba.

 Mashindano ya Lwakatare Cup hatua ya 16 bora yamesimamishwa kwa wiki moja kupisha ligi daraja la tatu kituo cha Mlimba kwa kushirikisha timu nne wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.

Msimamizi mkuu wa Lwakatare Cup 2017, kituo cha Mngeta, Supertus Duma alisema ligi daraja la tatu imesimamisha kuanza kwa michezo ya 16 bora ya Rwakatare Cup 2017 iliyokuwa imepangwa kwenye vituo saba.

Duma alisema michezo ya kwenye vituo imemalizika katikati ya juma ambapo timu 16 zitachuana na kubakia timu nane za kuingia robo fainali.

Alitaja timu zilizoingia 16 bora kuwa ni Teachers FC, Street Boys FC na Mlimba City FC kutoka kituo cha Mlimba wakati kituo cha Mngeta ni City Boys FC, Super Mahakama FC na Mngeta Rangers FC zilipenya huku kituo cha Chita ikitoa timu za Express FC na JKT Chita FC.

Nyingine ni Kidatu Kijiweni FC, Serengeti Boys kutoka kituo cha Mkamba, Mlabani FC, Shupavu FC kituo cha Ifakara, wakati kituo cha Namawala ni Idete FC na Namawala FC huku Mwaya B na Ichombe Star zikitoka kituo cha Mang’ula.

Duma alisema ligi daraja la tatu itaanza kutimua vumbi kituo cha Mlimba Oktoba 3 na itamalizika Oktoba 9 mwaka huu ikishirikisha timu nne za Super Mahakama FC, City Boys FC za Mngeta, Viwawa FC ya Malinyi na wenyeji Mlimba City FC.

Mashindano hayo yameshirikisha jumla ya timu 80 zilizopangwa katika vituo saba vya viwanja saba vya Mkamba, Mang’ula, Namawala, Ifakara, Chita, Mlimba na Mng’eta ambapo mshindi wa kwanza ataondoka na zawadi ya Sh2 milioni huku wa pili akipata Sh1milioni.

 “Viongozi wa TFF ngazi ya wilaya wanatakiwa kujenga utamaduni wa kufuatilia mashindano yasiyo rasmi hasa kwenye ligi za mchangani yanayochezwa zaidi vijiji ili kung’amua vipaji vya na kuwapeleka ligi za ngazi ya TFF watakaweza kuonekana na vilabu vikuwa.”alisema Duma.