Friday, September 22, 2017

Mabingwa watetezi Ligi Kuu Zanzibar waingia mzigoni -VIDEO

By Haji Mtumwa

Zanzibar. Nahodha wa JKU, Ponsiana Malik Joseph ametamba kutumia uwezo wake kuhakikishia timu yake hiyo inaendelea kutetea taji lake la ubingwa wa Ligi Kuu Zanzibar. 

Joseph alisema kuwa kikosi chake kinafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Saateni Mjini Unguja , ikiwa ni maandalizi ya Ligi Kuu ya Zanzibar inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi mwanzoni mwa mwezi ujao.

Alisema ana kila sababu ya kutamba kutwaa ubingwa huo ijapokuwa msimu ujao unaeonekana kuwa na upinzani mkali kwa baadhi ya vilabu navyo kujinoa kwa kasi.

“Tunatambua msimu mpya ni mgumu ila kwa upande wetu tumejiandaa na tunazidi kujiandaa vyema ili kuona tunatetea ubingwa wetu, miongoni mwa maandalizi hayo ni haya mazoezi,” alisema Joseph.

Joseph alisema mbali ya maamdalizi ya ligi hiyo lakini pia mazoezi hayo yatakuwa ni sehemu ya kujiandaa na mashindano ya Cecafa ambao wao watashiriki kama ni mabingwa wa Ligi Kuu  Zanzibar.

 

-->