Mchezaji avunjika mguu

Muktasari:

  • Kwa sasa anasubiri uchunguzi zaidi wa daktari ambaye atatoa hatima yake kuendelea na soka au kusubiri hadi atakapopona.

 

 Mwishoni mwa wiki iliyopita katika mchezo wa Ligi Daraja la Pili (SDL) kati ya AFC Arusha na Kitayosce, kipa wa Kitayosce, Mussa Juma alikumbana na majeraha yaliyomsababishia kutolewa nje.

Katika mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Ushirika na AFC kuibuka na ushindi wa bao 1-0, lililofungwa na John Milinye dakika 47, kipa huyo aligongana na mchezaji wa AFC Dickson Kalinga katika harakati za kuokoa hatari iliyokuwa inaelekea langoni mwake.

“Baada ya kuona maumivu makali ndipo uongozi wa timu uliponiwahisha Hospitari ya KCMC kwa matibabu zaidi na hatimaye daktari kugundua nimepata tatizo kwenye mfupa mdogo wa mguu wa kulia,” alisema Juma.

Aliongeza kuwa kwa sasa haruhusiwi kufanya lolote na baada ya wiki mbili atatakiwa kwenda kutazamwa tena hospitalini na hapo ndipo atakapojua mustakabali wake wa kukaa nje kwenye soka.