Malkia wa muziki wa soul afariki dunia

Muktasari:

  • Aretha Franklin alikuwa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa katika Rock na Hall of Fame, alifariki dunia huko Detroit, Marekani.

Detroit, Marekani. Mwanamuziki aliyetikisa katika muziki wa soul, hadi kuitwa malkia, Aretha Franklin amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 76.

Aretha Franklin alikuwa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa katika Rock na Hall of Fame, alifariki dunia huko Detroit, Marekani.

Mwanamuziki huyo alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa saratani tangu mwaka 2010 na alitangazwa kuwa anaumwa wakati akistaafu muziki mwaka jana.

Muziki wake ambao ulijulikana zaidi ulikuwa ni 'Respect and Think' ambao ulikuwa katika nyimbo 20 bora zilizopendwa zaidi nchini Marekani kwa miongo saba.

Mwanamuziki huyu alifanya onyesho lake la mwisho mwezi Novemba mwaka jana, katika ukumbi mmmoja mjini New York, akisaidiwa na taasisi ya mwanamuziki nyota wa Uingereza, Elton John ' Elton John Aids Foundation'.

Aretha aliyezaliwa Memphis, Marekani, alianza kuimba kama muimbaji wa dini na mpiga kinanda na alikuwa muhubiri katika sherehe za ubatizo.