Man United yampa masharti straika Martial

London, England. Klabu ya Manchester United imemuwekea masharti magumu mshambuliaji Anthony Martial.

Man United imesema mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa, hatauzwa katika klabu ya England.

Martial amewekwa sokoni baada ya kushindwa kupata namba katika kikosi cha kwanza.

Klabu ya Chelsea na Tottenham Hotspurs zimeonyesha dhamira ya kutaka saini ya Martial katika usajili wa majira ya kiangazi.

Martial mwenye miaka 22, alikuwa na kipindi kigumu msimu huu baada ya kucheza mechi chache akifunga bao la mwisho Januari, mwaka huu.

Kocha Jose Mourinho amekuwa na shauku ya kumsajili Willian ambaye amekuwa kwenye kiwango bora.

Martial, aliyetua Man United mwaka 2013 kutoka Monaco, alianza vyema katika kikosi kabla ya kupotea.

Klabu za Italia Napoli na Juventus ‘Kibibi Kizee’ cha Turin zimemtupia ndoano Martial zikitaka kumsajili majira ya kiangazi.