Manchester City, Bristol kuumizana Kombe la Carabao

Muktasari:

  • Fainali ya Kombe la Carabao inatarajiwa kupigwa mwezi ujao kwenye Uwanja wa Wembley.

England. Timu za Manchester City na Bristol City zinakutana kwa mara nyingune leo Jumanne ikiwa ni mara ya pili kwenye nusu fainali ya Kombe la Carabao.

Mchezo wa kwanza kikosi cha Kocha Pep Guardiola kilifanikiwa kuibuka naushindi wa mabao 2-1, ambapo ushindi wa leo kwa kila timu ni muhimu ili kujihakikishia kucheza fainali mwezi ujao kwenye Uwanja wa Wimbley.

Guardiola amesema kwamba anahitaji umakini zaidi kwa wachezaji wake ili kuhakikisha wanatwaa ubingwa wa mashindano hayo msimu huu.

Aliongeza kuwa anatarajia kupanga kikosi bora licha ya baadhi ya nyota wake kutocheza kama Brnardo Silva, Gundogan na Mangaka.

Wachezaji kama Yaya Tourem Brahimu Diaz na Okleksandr wanaweza kuwapo kwenye kikosi cha Pep Guardiola leo Jumanne usiku.

Mchezaji kiungo Zichenko mwenye miaka 21 ambaye amecheza mara sita katika msimu huo na amekuwa kiungo muhimu wa kushoto alicheza kikosi cha kwanza wakati timu yake ilipokutana na Newcastle Jumapili iliyopita.