Nyota wa Hollywood kutangaza tuzo ya Fifa

Muktasari:

  • Neymar anajaribu kwa mara pili kusaka tuzo hiyo wakati Ronaldo na Messi wamechukua kwa kupokezana tuzo hiyo tangu 2009

Shirikisho la Soka Duniani Fifa limetangaza mwingizaji Hollywood, Idris Elba atakuwa mtangazaji wakati sherehe za kutangazwa tuzo za mwanasoka bora wa Fifa kesho, Jumatatu.

Elba ambaye aliingiza kama Nelson Mandela katika filamu ya "Mandela: Long Walk to Freedom", pia filamu ya “Sometimes in April” ya mauji ya kimbari Rwanda na mshindi wa Golden Globe mwaka 2012 pia ni tangazaji wa kipindi cha TV "Luther," atakuwa mtangazaji katika hafla hiyo itakayofanyika London Palladium.

Nyota huyo mwenye miaka 44, ni shabiki mkubwa wa Arsenal amezaliwa London, ataungana na mtangazaji wa ESPN, Layla Anna-Lee huku bendi ya Kasabian ikitumbuiza katika hafla hiyo.

Mshindi wa mwaka jana, Cristiano Ronaldo anapewa nafasi kubwa ya tetea taji lake dhidi ya washindani wake Lionel Messi na Neymar.

Kocha wa Ronaldo katika kikosi cha Real Madrid, Zinedina Zidane anawania tuzo ya kocha bora wa mwaka wa Fifa pamoja na bosi wa Juventus, Massimiliano Allegri na kocha wa Chelsea, Antonio Conte.

Mchezaji timu ya taifa ya wanawake wa Marekani, Carli Lloyd atakuwa akitetea tuzo yake ya mchezaji bora wa mwaka kwa wanawake dhidi ya nyota wa Venezuela, Deyna Castellanos na Lieke Martens wa Uholanzi.

Castellanos pia anawania tuzo bao bora la mwaka Puskas dhidi ya mshambuliaji wa Arsenal, Olivier Giroud pamoja na kipa wa Afrika Kusini, Oscarine Masuluke.