Liverpool yaichakaza Porto kwao

Muktasari:

  • Liverpool ni bingwa mara tano wa Ligi ya Mabingwa alitwaa ubingwa huo mara ya mwisho 2005

London, England. Mshambuliaji wa kimataifa Senegal, Sadio Mane, amepiga mabao matatu ‘hat-trick’, na kuiongoza Livepool kuichakaza Porto kwa mabao 5-0 katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Vijana wa Jurgen Klopp wameendeleza rekodi ya kufunga mabao mengi msimu huuwakati washambuliaji wake watatu Mane, Mohamed Salah na Roberto Firmino kila moja alifunga goli na kufanya mchezo wao wa marudiano Anfield kuwa mwepesi kidogo kwao.

Mane alifunga bao la kwanza dakika ya 25, kwa kutumia vizuri uzembe wa kipa Jose Sa, kipa huyo wa Porto alikosema kucheza mpira uliopigwa na Georginio Wijnaldum.

Liverpool walipata bao la pili kupitia kwa Salah na kufanya kuwa mchezaji wa kwanza wa Liverpool kufunga mabao 30, tangu alipofanya hivyo Luis Suarez katika msimu wa 2013-14.

Washambuliaji hao watatu wa Liverpool walichangia kupatikana bao la tatu na la pili kwa Mane, naye Firmino alifunga bao lake zikiwa zimebaki dakika 21 kabla ya mpira kumalizika.

Bado kulikuwa na muda kwa Mane kuhitimisha kwa kwa kufunga bao la tatu na kuacha matumaini madogo kwa Porto kufuzu kwa hatua katika mechi ya marudiano.

“Kocha amekuwa akinitumia kucheza nafasi ya winga wa kushoto ingawa nafasi ya kulia, lakini kokote nacheza,” alisema Mane.

Klopp aliendelea kumuamini libero ghali duniani Virgil van Dijk kwa kumpa nafasi ya kuongoza katika safu ya ulinzi.

Beki huyo raia wa Uholanzi, amekuwa akiandamwa na baadhi ya wachambuzi wa soka akiwemo Carragher wakipondam bei aliyonunuliwa na ubora wake.

Van Dijk ametua Liverpool kwa Pauni 75 milioni kutoka Southampton ‘Watakatifu’ katika usajili wa dirisha dogo mwezi uliopita.

Mane anakuwa mchezaji wa pili Liverpool kufunga mabao matatu katika mchezo mmoja wa  baada ya Michael Owen aliyefunga dhidi ya Haka mwaka 2001 na Spartak Moscow 2002.