Masalia Simba, Yanga kusajili Madini SC

Muktasari:

Meneja wa timu hiyo Bakari Kigodeko alisema wamefanikiwa kupata wachezaji wa mkopo kutoka Simba, Yanga, Azam, Ashanti United pamoja na Mtibwa Sugar hivyo kufanya kuwa na kikosi kipana huku Simba wakiwapa wachezaji sita, Yanga wanne, Azam wawili.

Arusha: Uongozi wa Timu ya Madini SC inayoshiriki ligi daraja la pili (SDL) umepa msimu ujao kupanda ligi daraja la kwanza (FDL) kwa kuhakikisha wanasajili wachezaji wenye uzoefu kutoka katika klabu kubwa.

Meneja wa timu hiyo Bakari Kigodeko alisema wamefanikiwa kupata wachezaji wa mkopo kutoka Simba, Yanga, Azam, Ashanti United pamoja na Mtibwa Sugar hivyo kufanya kuwa na kikosi kipana huku Simba wakiwapa wachezaji sita, Yanga wanne, Azam wawili.

Licha ya kutowataja majina wachezaji hao wanaotarajia kutua mwishoni mwa wiki hii kabla ya kuanza mazoezi rasmi wiki ijayo baada ya timu nzima kuingia kambini.

Katibu Mkuu wa timu hiyo, Zephrine Karunde alisema wanamikataba na wachezaji 20 hivyo watakaoingia kambini ndio wenye nafasi ya kuboresha mkataba yao huku nafasi zilizobaki wataziba kwenye dirisha la usajili linaloendelea.

Aliongeza katika kuhakikisha wanakuwa na benchi imara la ufundi ndio maana Mkongwe Bakari Kigodeko amekuwa meneja wa timu badala ya kuwa kocha msaidizi msimu uliopita huku kocha Mkuu akibaki Abdalah Juma.

“Tuliona mchango mkubwa wa Kigodeko msimu uliopita, lakini tumeamua kuongeza wigo wa madaraka ili iwe rahisi katika kuboresha kikosi hasa nyakati hizi za usajili kwani timu ina mambo mengi,” alisema Karunde.