Mashabiki kiduchu wajitokeza kuiona Yanga, Njombe Mji

Muktasari:

Yanga imeshuka dimbani leo kucheza mechi ya pili katika mzunguko wa pili huku ikiwa imeanza vyema mechi ya kwanza dhidi ya Lipuli FC.

Dar es Salaam. Mashabiki wameonekana kuingia kwa kusuasa kwenye Uwanja wa Uhuru kuziona Yanga na Njombe Mji kwenye mechi ya Ligi Kuu inayochezwa leo Jumanne.

Yanga imeshuka dimbani leo kucheza mechi ya pili katika mzunguko wa pili huku ikiwa imeanza vyema mechi ya kwanza dhidi ya Lipuli FC.

Kocha Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa amesema kikosi chake kipo tayari kuivaa Njombe Mji baada ya kazi nzito ya Iringa dhidi ya Lipuli.

Hata hivyo majukwaa mengi kwenye uwanja huo yalionekana kuwa wazi kutokana na kuwapo mashabiki wachache waliojitokeza.