Mashabiki wafurika uwanjani kabla ya mechi ya Simba v Mbao FC

Muktasari:

  • Mechi hiyo yenye ushindano inatarajiwa kuchezwa leo Alhamisi saa 10 jioni, huku mashabiki wakiwa nje ya uwanja kabla ya mageti kufunguliwa.

Mwanza. Mashabiki wa soka jijini Mwanza wamefurika kupanga foleni kwa jili ya kuingia uwanjani ili kuishuhudia mechi ya Simba na Mbao FC inayotarajiwa kupigwa leo kwenye dimba la CCM Kirumba  jijini hapa.

Mechi hiyo yenye ushindano inatarajiwa kuchezwa leo Alhamisi saa 10 jioni, huku mashabiki wakiwa nje ya uwanja kabla ya mageti kufunguliwa.

Mpambano huo wa leo utatoa majibu kwa Simba kukalia kiti kileleni au la.