Mashabiki wakoleza mbizo za ubingwa wa Simba

Muktasari:

Kwa ushindi wa jana, Simba inaendelea kuongoza na pointi 41, Yanga 34, Azam 33 na Singida 30.

KIKOSI Simba kimeonyesha kutwaa ubingwa baada ya kuichapa Azam FC bao 1-0 mchezo uliopigwa jana Jumatano.

Emanuel Okwi ndiyo alikuwa shujaa wa mchezo kwani ndiye alifunga bao hilo pekee dakika ya 36 akiunganisha pasi ya Said Ndemla.

Mlinda mpango wa Azam, Razack Abalora alijitahidi kuokoa michomo ya Simba Mara kwa Mara lakin mambo hayakuwa mazuri.

Ushindi huo umeibua hamasa mpya kwa mashabiki kuwa na matumaini wa timu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi kuwa kwenye nafasi ya kutwaa ubingwa iwapo itaendeleza kasi hiyo hadi mwisho.

Emmanuel Okwi alisababisha mashabiki waliokuwapo uwanjani hapo kushangilia wakat wote kuonyesha kuwa safari waliyoanza ya kusaka taji, wamedhamiria kuikamilisha.