Mashindano ya gofu ya MCL- LBGC yapamba moto Lugalo

Muktasari:

Wachezaji nyota wa kike, Angel Eaton, Hawa Mwanyenche, Vicky Elias, Maryanne Hugo na  Priscilla Karobia walikuwa mingoni mwa wachezaji maarufu walioshindana  katika mashindano hayo yaliyosimamiwa na  Godfrey Kilenga.

Dar es Salaam. Mashindano ya gofu maarufu kwa jina la Breakfast Golf Community tournament (MCL-LBGC) yameshirikisha jumla ya wacheza gofu maarufu 42 nchini.

Mashindano hayo yaliyoanza saa 7.00 mchana jana Ijumaa, yamedhaminiwa na Mwananchi Communications Limited (MCL), kampuni inayochapisha magazeti ya The Citizen, Mwananchi na Mwanaspoti.

Wachezaji nyota wa kike, Angel Eaton, Hawa Mwanyenche, Vicky Elias, Maryanne Hugo na  Priscilla Karobia walikuwa mingoni mwa wachezaji maarufu walioshindana  katika mashindano hayo yaliyosimamiwa na  Godfrey Kilenga.

Wachezaji wengine maarufu wa kiume ni Martin W, John H, Simon Kaphale, Femin Mabachi, Joseph Tango, Mohamed Rweyemamu, Godfrey Kilenga, Foti Gwebe, Fred L, Cloudy Mtavangu, Pro. Nyenza na Gilman K.

Wachezaji wengine ni  Mwanyenza S, Letara M, Noel M, Torence M, Amanzi Mandengule, Boniface Nyiti,  Ali Mufuruki, Tairo J, Michael Kaire, Magile E, Chasosa I, Alex N, Balozi Kalino, Zacharia Edward, Kajuna M, Prof Nyirabu, Francis Ekeng, Mwinuka F, Japhet M,  Magige W, Samwel M na  Prosper Emmanuel.

“Maandalizi yamekamilika na wachezaji wote wapo katika morali ya hali ya juu kwa ajili ya kuonyesha uwezo wao katika mashindano ambayo yamepangwa kuanza saa 6.00 mchana na kumalizika jioni. Tumeandaa utaratibu mzuri kwa kila mchezaji ili kuweza kufanya mashindano kwa ufanisi mkubwa,” alisema Kilenga.

Meneja Masoko wa MCL, Sarah Munema alisema kuwa wameamua kudhamini mashindano hayo ili kuleta hamasa na maendeleo ya mchezo huo mbali ya kujishughulisha na shughuli za kijamii.

Munema alisema wanatambua umuhimu wa mchezo huo na vilevile watatumia fursa hiyo kukutana na wateja wao, jujadili masuala mbalimbali mbali ya kucheza gofu.