TFF yamfungia maisha Wambura

Muktasari:

  • Kiongozi huyo wa Mara aliwahi kufungiwa kugombea nafasi yoyote ndani ya TFF kwa zaidi ya miaka tisa

Dar es Salaam. Makamu wa Rais wa Shirikisho Soka la Tanzania (TFF), Michael Wambura amefungiwa kutojihusisha na masuala ya soka maisha baada ya kukutwa na hatia,na Kamati ya Maadili ya TFF iliyokutana jana na kufikia hatua hiyo.

Afisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo alisema kamati hiyo iliyokaa jana ikiongozwa na Mwenyekiti wake Hamidu Ally Mbwezereni, wamemkuta na makosa matatu yatakayomfanya Wambura asijihusishe na masuala ya soka.

Kosa la kwanza amevunja kifungu no 73 kwa kupokea malipo yasiyo halali ya TFF, ambapo faini yake ni milioni 10, kutojihusisha na soka miaka mitano au maisha.

Kosa la pili kugushi malipo kwa jina la TFF enzi hizo (FAT), ambapo amezuiliwa kujihusisha na soka kwa miaka 5.

Kosa la tatu linalomkabili ni kushusha hadhi ya TFF, kosa ambalo adhabu yake iliyotolewa ni kutojihusisha na soka maisha.