Lukaku, Kompany waendeleza undugu baada ya kipigo

Muktasari:

Mchezo wa Manchester United vs Manchester City uligubikwa na malalamiko kutoka kwa makocha wa pande zote kulalamikia uamuzi wa uwanjani.

England. Nyota wa Manchester United, Romelu Lukaku na mwenzake wa Manchester City, Vincent Kompany ambao ni raia wa Belgium, hawakausita kusalimiana licha ya timu zao  kufanyiana ubabe uwanjani.

Mechi hiyo iliisha kwa Manchester City kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya kikosi cha Jose Mourinho, lakini matokeo ya uwanjani  hayakuwa kikwao kwa mastaa hao kupeana mikono.

Licha ya Mourinho kuonekana akilalamika kwenye mchezo huo kutokana na kutoridhisha na maamuzi uwanjani, lakini Lukaku hakuonyesha tofauti yoyote kwa mchezaji mwenzake wa Belgium, Kompany baada ya mpira kumalizika.