Masumbwe Worriors yaiadhiri Ushirombo FC

Muktasari:

Ligi hiyo inachezwa kwa mtindo wa mtoani huku mtanange huo ulipigwa katika uwanja wa Mabatini ambapo ndani ya dakika 90 timu hizo zilitoka
sare ya 1-1.

Masumbwe Worriors kama kawaida yao imeichapa Ushirombo Rangers kwa mikwaju ya penalti ya 5-4 katika mchezo wa Ligi ya Chale Cup uliopigwa juzi wilayani Mbogwe.

Ligi hiyo inachezwa kwa mtindo wa mtoani huku mtanange huo ulipigwa katika uwanja wa Mabatini ambapo ndani ya dakika 90 timu hizo zilitoka
sare ya 1-1.

Ushirombo ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao ambalo liliwekwa kimiani na mshambuliaji Jamhuri Nestory dakika ya 12.

Hata hivyo vijana wa Masumbwe walipambana na kufanikiwa kusawazisha bao dakika ya 60  kupitia kwa straika wake, Benjamini Ernest.

Baada ya dakika hizo 90 kumalizika pasipo kumpata mshindi ndipo ilipoamriwa ipigwe mikwaju hiyo ya penalti ambapo Masumbwe waliwapata
tano huku Ushirombo wakifunga nne.

Mratibu wa Ligi hiyo, Charles Francis alisema bingwa wa michuano hiyo atapata Sh1 milioni na seti moja ya jezi, mshindi wa pili akipata Sh700,000 na seti ya jezi huku wa tatu  Sh500,000.

“Ligi inachezwa kwa mtindo wa mtoani kwa mana ukifungwa mchezo mmoja
ndio umetoka na mwenzako anasonga mbele,”alisema.