#WC2018: Balozi anataka hili Taifa Stars iwe na kina Poulsen wengi

Muktasari:

Jensen ambaye ni mfualitiaji mzuri wa mashindano ya kombe la Dunia Russia, ameisifu Tanzania kwa kusema inaweza kuwa na timu bora ya taifa kama watazingatia misingi ya mchezo huo.

Dar es Salaam. Balozi  wa Denmark nchini,  Einar Jensen amesema wingi wa vituo bora vya soka  vinaweza kuwaibua wakina, Yussuf Poulsen wengi watakaolibeba taifa la Tanzania katika mchezo huo.

Jensen ambaye ni mfualitiaji mzuri wa mashindano ya kombe la Dunia Russia, ameisifu Tanzania kwa kusema inaweza kuwa na timu bora ya taifa kama watazingatia misingi ya mchezo huo.

“Poulsen ni mchezaji mzuri ambaye ameionyesha Dunia kuwa Tanzania ni moja ya mataifa ambayo yanapaswa kuangaliwa lakini ubora wake umeonekana kwa sababu amekuwa kwenye misingi ya mpira," Jensen.

“Denmark ina akademi nyingi ambazo zimekuwa zikiandaa  vijana wa uhakika, sio akademi za kupita hapa na ni zenye viwango vya juu, kila mahali kuna watu wahususi ambao kazi yao ni kuangalia vijana wenye vipaji mitaani,” alisema Balozi huyo.

Balozi huyo, ameongeza kuwa miongoni mwa vitu vya msingi ambavyo wachezaji wa kiwango cha mshambuliaji wa Denmark mwenye asili ya Tanzania, Poulsen  vimekuwa vikiwabeba  ni  nidhamu.

Poulsen anategemewa kuiongoza tena Demark leo kwenye mchezo wao wa pili wa kombe la Dunia dhidi ya Australia ambao utachezwa majira ya saa 9: 00 alasiri kwa muda wa  Afrika Mashariki.