Liverpool, Man City wasubiri wabaya wao Ulaya
Muktasari:
- England ilikuwa na timu tano katika hatua ya 16 bora zimetoka tatu na kubaki mbili tu
Liverpool, Manchester City na vigogo Ulaya wanajiandaa kwa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa itakayopahwa mjini Nyon leo mchana.
Liverpool na Manchester City ndiyo timu pekee zinazopeperusha bendera ya Ligi Kuu England pia kuna uwezekano wa kucheza wenyewe.
Kuanzia hatua hii ratiba ipo wazi kwa timu za nchi moja kukutana au kucheza na timu uliyokuwa nayo kundi moja.
Timu nane zilizosalia katika mashindano hayo ukiangalia rekodi yao na mafanikio katika mashindano hayo:
BARCELONA
Lionel Messi ndiyo tishio zaidi akisaidiwa na Luis Suarez. Kwa sasa wanaongoza La Liga kwa tofauti ya point inane hivyo wanaweza kuweka akili yao katika Ligi ya Mabingwa zaidi.
Kocha: Ernesto Valverde
Mchezaji Nyota: Lionel Messi
Mafanikio yao: Ubingwa 1992, 2006, 2009, 2011, 2015.
BAYERN MUNICH
Kocha Jupp Heynckes ametwaa taji hili akiwa na Real Madrid na Bayern. Sasa anataka kunyakuwa taji hilo kwa mara ya tatu.
Kocha: Jupp Heynckes
Mchezaji Nyota: Robert Lewandowski
Mafanikio yao: Ubingwa 1974, 1975, 1976, 2001, 2013
JUVENTUS
Pamoja na kushindwa kuonyesha kiwango cha kuridhisha dhidi ya Tottenham, lakini wamefanikiwa kusonga mbele.
Kocha: Massimiliano Allegri
Mchezaji Nyota: Paulo Dybala
Mafanikio yao: Ubingwa 1985, 1996
LIVERPOOL
Walikuwa bora zaidi kwa Porto wamefuzu kwa hatua hiyo wakiwa na rekodi ya kutopoteza mechi hadi sasa. Washambuliaji wake watatu Mo Salah, Roberto Firmino na Sadio Mane wamefunga kila mechi.
Kocha: Jurgen Klopp
Mchezaji Nyota: Mohamed Salah
Mafanikio yao: Ubingwa 1977, 1978, 1981, 1984, 2005
MAN CITY
Kocha Pep Guardiola amethibisha ubora wake kwa kutegeneza timu ya ushindi. Tayari wanakaribia ubingwa wa Ligi Kuu England, hivyo akili ya City sasa ni kutamba Ulaya.
Kocha: Pep Guardiola
Mchezaji Nyota: Kevin De Bruyne
Mafanikio yao: Nusu fainali 2016
REAL MADRID
Swali kuhusu hatma ya Zinedine Zidane, litasahaulika kama atafanikiwa kutwaa taji la tatu mfululizo.
Kocha: Zinedine Zidane
Mchezaji Nyota: Cristiano Ronaldo
Mafanikio: Ubingwa 1956, 1957, 1958, 1959, 1960, 1966, 1998, 2000, 2002, 2014, 2016, 2017
ROMA
Baada ya kuondolewa hatua hiyo dhidi ya Chelsea na Atletico Madrid, safari hii imevunja mwiko kwa kuichapa Shakhtar kwa sheria ya bao la ugenini katika hatua ya 16 bora.
Kocha: Eusebio Di Francesco
Mchezaji Nyota: Edin Dzeko
Mafanikio yao: Washindi wa pili 1984
SEVILLA
Mara ya mwisho kufuzu kucheza robo fainali ilikuwa 1958, Sevilla wamerudi upya baada ya kuiondoa Manchester United.
They are not the side that won three straight Europa Leagues but have responded well to former AC Milan boss Vincenzo Montella.
Steven N’Zonzi is the midfield powerhouse and Wissam Ben Yedder, who scored two against United, has been a real surprise package.
Kocha: Vincenzo Montella
Mchezaji Nyota: Wissam Ben Yedder
Mafanikio Yao: Robo fainali 1958, 2018