Messi afanya yake Stamford Bridge

Muktasari:

  • Mechi ya marudiano itachezwa kwenye Uwanja wa Camp Nou, Machi 14.

Mshambuliajia wa Barcelona, Lionel Messi, ameivunja rekodi ya kutofunga bao dhidi ya Chelsea pindi timu hizo zinapokutana akiwa na timu yake.
Messi tangu aanze kuichezea Barcelona mpaka kabla ya mchezo wa jana, hakuwahi kuzigusa nyavu za Chelsea.
Iniesta ndiye alimsaidia Messi kufunga bao hilo kwa pasi safi ikitokea upande wa kushoto mwa Uwanja wa Stamford Bridge.
Bao lake la kusawazisha limekuwa muhimu kwa Barcelona ambayo imekuwa na faida ya goli moja la ugenini, kabla timu hizo hazijakutana tena katika mchezo wa marudiano.