Tuesday, March 13, 2018

Yanga yawatambia Waswana, wasema wataumia tu

 

By DORIS MALIYAGA

MSHAMBULIAJI chipukizi wa Yanga, Yusuph Mhilu amesema, wameondoka kwenda Botswana wakiwa na matumaini ya kuwafunga wapinzani wao Township hukohuko kwao.

Mhilu amesema, licha ya kuwa wanaenda huko wakiwa nyuma kwa bao moja baada ya kufungwa mabao 2-1 mechi ya awali, anaimani mapambano watakayopambana lazima watapa matokeo mazuri.

"Tunakwenda kupambana na kuhakikisha tunapata matokeo mazuri huko huko Botswana kwa sababu kila kitu kinawezekana kikubwa ni kujituma tu. Haijalishi tutacheza ugenini au nyumbani kwa sababu hata wao walikuja kwetu wakashinda na sisi tunakwenda kwao tutashinda tu,"anasema Mhilu na kuwaomba Watanzania wote haswa wale mashabiki wa Yanga kuiombea timu hiyo ikapate matokeo.

Yanga na Township watacheza Jumamosi hii nchini Botswana mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika,  ukiwa ni mchezo wa awamu ya pili wa marudiano baada ya kufungwa mabao 2-1 Uwanja wa Taifa.

-->