Milioni 80 zamsubiri Yondani Simba

Muktasari:

  • Beki huyo anataka sh 80 milioni ili asaini mkataba Simba

Nairobi, Kenya. Beki wa Yanga, Kelvin Yondani wakati wowote anaweza kujiunga na Simba kwa uhamisho wenye thamani ya Sh 80milioni.

Yondani hakuambana na Yanga kwenda Nairobi kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahi utakaochezwa kesho kwenye Uwanja Kasarani, Kenya.

Taarifa ilizozipata MCL Digital zinadai kuwa Yondani leo alikutana na viongozi wa Simba kuhusu kumsajili na kuna uwekezano kwenda kuonana na Mohammed Dewji 'MO' kesho asubuhi.

Chanzo hicho kimedai kuwa beki huyo Yondani ametaka kupewa Sh 80 milioni ili kusaini mkataba wa kujiunga na Simba.

Iko hivi,  mmoja wa Wajumbe wa kamati ya usajili Simba (Jina lake tunayo) ndio alipewa jukumu hilo zito la kuzungumza na Yondani ili asaini Simba.

Katika mazungumzo hao hayakufikia muafaka kwani Yondani alisema bila Sh80 Milioni hawezi kusaini hapo.

"Kesho (leo) saa nne kuna uwezekano tukaenda naye kwa MO na kama tutakubaliana kati yetu na yeye tunaweza kumpa mkataba.

"Mwenyewe alitaka Sh 80 Milioni ili asaini na miaka miwili, lakini tulishindwa kukamilisha ila baada ya kesho nadhani tutatoka na majibu kamili, " alidai Mjumbe huyo.

Yondani ameshindwa kusaini mkataba mpya Yanga akishindikiza kumlipa fedha zake anazotaka ili kuendelea kuichezea timu hiyo.

Tangu mwisho wa msimu uliopita, Yondani amekuwa akihusishwa na kutakiwa na Simba hiyo ni kutokana na uamuzi wake wa kujitoa katika kikosi kilichocheza mechi mbili za awali wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga ilimsajili Yondani kutoka Simba mwaka 2012 akiwa katika kambi ya timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, jambo lililozua mzozo mkubwa baina ya TFF na Simba.

Mkongo atia neno kwa Yondani

Kocha Mkongomani wa Yanga, Mwinyi Zahera alisema kweli timu inapitia kipindi kigumu ndio maana wanawakosa baadhi ya wachezaji muhimu.

Zahera alisema Uongozi wa Yanga unafanya kazi nzuri na mambo yote yataisha na timu kurudi katika mstari mnyoofu.

"Kweli Kuna baadhi ya wachezaji wataondoka, lakini walikuwa muhimu kwetu ila mambo tu kutokukaa sawa ndio tumeshindwana kuwabakisha lakini kama timu tutasajili wengine wazuri," alisema Zahera.

Kocha msaidizi wa Yanga, Noel Mwandila alisema mchezaji yoyote hata kama alikuwa na umuhimu kwetu kama tulishindwa kukabiliana na kumpa mkataba mpya nimtakie kila la kheri huko endapo.