Missanga kuagwa leo, kuzikwa kesho Singida

Muktasari:

  • Marehemu aliongoza mapinduzi makubwa Yanga katika mwaka 1976

 Makamu Mwenyekiti wa zamani wa chama cha Soka Tanzania (FAT) sasa TFF, Mohamed Missanga ataagwa leo Desemba 11 nyumbani kwake Mikocheni na kuzikwa kesho Singida.

Missanga alifariki alfajiri ya Desemba 10 kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili kitengo cha Moyo alipokuwa amelazwa akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo.

Akizungumzia msiba huo, rafiki wa marehemu, Ismail Aden Rage alisema ataagwa leo nyumbani kwake eneo la Regent Estate, Dar es Salaam.

"Marehemu atazikwa Jumanne 'kesho' kijijini kwao Ititi huko Singida, safari ya kuelekea Singida itaanza saa 10 jioni leo baada ya ibada ya kumuaga nyumbani kwake," alisema Rage.

Missanga amewahi kuwa katibu mkuu wa Yanga enzi za uhai wake, pia Mbunge wa Singida Kusini.